• info@tas.or.tz
  • +255743803141 743 803 141
/

TAS Yaelimisha Jamii Kupitia Filamu JIKUBALI Shule ya Msingi Sanze

Mratibu wa Miradi wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) akitoa ufafanuzi kuhusu maudhui ya filamu JIKUBALI, filamu inayolenga kuonesha na kuhamasisha jamii kuhusu mafanikio ya watu wenye ualbino katika nyanja mbalimbali za maisha.

Tukio hilo lilifanyika katika Shule ya Msingi Sanze, shule jumuishi iliyopo Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, likihusisha wanafunzi, walimu na wadau wa elimu, kwa lengo la kuongeza uelewa, kuondoa unyanyapaa na kuhimiza kukubaliana na kuthamini utofauti katika jamii.