• info@tas.or.tz
  • +255743803141 743 803 141
/

TAS Yaandaa Warsha ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano

Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) kupitia Makao Makuu kimeandaa warsha maalum ya kuandaa Mpango Mkakati wa TAS wa miaka mitano, ikiwahusisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali nchini pamoja na wadau muhimu wa chama.

Warsha hiyo imewakutanisha wajumbe wa bodi, wafanyakazi wa TAS, Wazazi, Idara ya Wanawake, Vijana, Wanachama pamoja na Wadau wengine, kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati itakayosaidia kuimarisha utekelezaji wa shughuli za TAS katika kipindi kijacho.

Kupitia warsha hiyo, washiriki wamepata nafasi ya kutoa maoni, mapendekezo na uzoefu wao ili kuhakikisha mpango mkakati unaandaliwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya watu wenye ualbino na maendeleo ya chama kwa ujumla.