• info@tas.or.tz
  • +255743803141 743 803 141
/

TAS Yatoa Vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Ushonaji

TAS imeendesha hafla ya utoaji wa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ufundi cherehani waliopata ufadhili kupitia mradi wa Kesho Angavu unaofadhiliwa na ActionAid Tanzania.

Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha vijana wenye ualbino kujitegemea kiuchumi kupitia ujuzi wa ufundi cherehani na kuongeza fursa za ajira na maendeleo katika jamii.