April 26, 2026
/
TAS Yapokea Wageni kutoka Sweden katika Kikao cha Mradi wa Elimu Jumuishi na Afya Bora
Viongozi na wafanyakazi wa TAS wamepiga picha ya pamoja na wageni kutoka Sweden wa taasisi za MyRight na SRF baada ya kikao cha mwaka cha mradi wa Elimu Jumuishi na Afya Bora kwa watu wenye ualbino.
Mradi huo unatekelezwa katika wilaya za Mafia, Nyasa, Kiteto na Kigoma Mjini, ukiwa na lengo la kuimarisha upatikanaji wa elimu jumuishi pamoja na huduma bora za afya kwa watu wenye ualbino katika jamii.