February 4, 2026
/
TAS Yashiriki Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani
Leo, Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) kimeshiriki katika matembezi ya kuadhimisha Siku ya Saratani Duniani, yenye kauli mbiu “United by Unique”. Ushiriki huu ulilenga kuonesha mshikamano katika mapambano dhidi ya saratani, kuongeza uelewa wa jamii kuhusu ugonjwa huu, pamoja na kuhamasisha umuhimu wa kinga, uchunguzi wa mapema na usaidizi kwa waathirika wa saratani, hususan watu wenye ualbino ambao wako katika hatari kubwa ya saratani ya ngozi.