April 26, 2026
/
TAS na ActionAid Wajadili Mafanikio ya Mradi wa Kesho Angavu
Viongozi wa TAS Taifa kwa kushirikiana na ActionAid pamoja na viongozi wa TAS Kwimba wamekutana kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mradi wa Kesho Angavu kwa watoto wenye ualbino.
Mkutano huo ulitoa nafasi ya kutathmini hatua zilizofikiwa, kujadili changamoto mbalimbali, na kuweka mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa mradi ili kuendelea kuboresha ustawi na maendeleo ya watoto wenye ualbino katika jamii.