April 26, 2026
/
TAS na ActionAid Watathmini Utekelezaji wa Mradi wa Kesho Angavu Mwanza
TAS kwa kushirikiana na ActionAid Tanzania wamefanya kikao mkoani Mwanza kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa mradi wa Kesho Angavu unaofadhiliwa na ActionAid Tanzania.
Kikao hicho kilihusisha viongozi na wadau mbalimbali kujadili mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza, pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa mradi ili kuendelea kuboresha maisha na ustawi wa watoto wenye ualbino.